Sunday, August 25

BOBI WINE AKAMATWA NA KUPELEKWA KUSIKOJULIKANA

0


Kampala, UGANDA.

Mwanamuziki maaarufu nchini Uganda na Mbunge Jimbo la Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine amekamatwa baada ya kukabiliana na vikosi vya usalama alipokuwa akijielekeza kufunguwa tamasha lake la muziki la sikukuu ya pasaka na kupelekwa kusikojulikana.

Purukushani hizo zilitokea baada ya maafisa wa polisi kuuzuia msafara uliokuwa ukiongozwa na Bobi wine katika tamasha lake la One Love katika eneo la Busabala nchini humo, tamasha ambalo lilipigwa marufuku na mamlaka nchini Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na gazeti la Daily Monitor la nchini humo, waandalizi wa tamasha hilo pia wamekamatwa ikiwa ni pamoja na mbunge wa jimbo la Makindye Magharibi, Mh Allan Ssewanyana.

Kwa mujibu wa mashahidi Bobi Wine alikamatwa na kuingizwa katika gari la polisi na kupelekwa eneo lisilojulikana, lakini mwanamuziki Nubian Li ambaye alikuwa akiongozana naye katika gari moja hakukamatwa.


Share.

About Author

Leave A Reply