Sunday, August 18

DK MSOLLA NJIA NYEUPE UENYEKITI YANGA BAADA YA MASHAURI NA DK. TIBOROHA KUJITOA

0


DK MSOLLA NJIA NYEUPE UENYEKITI YANGA BAADA YA MASHAURI NA DK. TIBOROHA KUJITOA – BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINEDK MSOLLA NJIA NYEUPE UENYEKITI YANGA BAADA YA MASHAURI NA DK. TIBOROHA KUJITOA – BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA wa zamani wa Taifa Stars, Dk Mshindo Msolla atapambana na Elias Mwanjala pekee kuwania Uenyekiti wa klabu ya Yanga katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Mei 5, mwaka huu mjini Dar es Salaam.
Hiyo ni baada ya mpinzani wake mwingine, Lucas Mashauri aliyekuwa anapewa nafasi kubwa ya kushinda kuenguliwa kutokana na kutojitokeza kwenye usaili, kufuatia Dk. Jonas Benedict Tiboroha, Mbaraka Hussein Igangula na Erick Ninga waliochukua fomu awali nao kujitoa.
Taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya Yanga inayoshirikiana na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wamepitishwa wagombea wawili pia.

Dk Mshindo Msolla atapambana na Elias Mwanjala pekee kuwania Uenyekiti wa Yanga Mei 5


Hao ni Katibu wa zamani wa TFF, Frederick Wilfred Mwakalebela na Mbunge wa jimbo Ileje (CCM) Mheshimiwa, Janet Zebedayo Mbena baada ya Samuel Lukumay na Thobias Lingalangala kuenguliwa kwa pingamizi, kufuatia Yono Kevela, Titus Eliakim Osoro na Salum Magege Chota kujitoa.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Wenyekiti wote wa Kamati za Uchaguzi, Mawakili Malangwe Mchungahela wa TFF na Sam Mapande wa Yanga imesema kwamba wagombea tisa tu wamepitishwa kuwania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.
Hao ni Dominick Albinus, Saad Mohamed Khimji, Hassan Yahya Hussein, Shafiru Amour Makosa, Mhandsi Bahati Faison Mwaseba, Hamad Ali Islam, Mhandisi Leonard Marangu, Suma Mwaitenda na Haruna Hussein Batenga.   
Na hiyo ni baada ya wagombea wengine kujitoa, ama kuenguliwa kwa mapingamizi au kutokukidhi vigezo baada ya usaili jana wakiwemo Siza Augustino Lymo, Tobias Lingalangala, Samuel Lukumay na Hussein Nyika.
Wengine waliojiuzulu katika uongozi wa Yanga uliongia madarakani Juni 11 mwaka ni aliyekuwa Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wanne, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Hashim Abdallah.
Share.

About Author

Leave A Reply