Sunday, August 18

Waandishi wafundwa ili kuendelea kuaminika

0
Mwenyekiti wa muda wa JOWUTA Said Mmanga akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo 
IMEELEZWA kuwa, taaluma ya habari itaendelea kuwa na heshima na kuaminika kwa jamii iwapo tu waandishi wa habari watakuwa na maslahi mazuri na mazingira bora ya kazi.
 Hayo yamebainishwa na washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya usawa wa kijinsia na mbinu za kufanyakazi katika mazingira hatarishi kwa waandishi wa habari mkoa wa Morogoro.
 Mafunzo hayo yameendeshwa na Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo Vya Habari (JOWUTA) kwa kushirikiana na chama cha wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini Norway na Shirika la Kimataifa la wana habari (IFJ). Kwa sasa JOWUTA ipo katika hatua za mwisho kupata usajili wa kudumu.
 Washiriki hao wamebainisha kuwa, kukosekana kwa chama cha wafanyakazi kwa waandishi wa habari kumechangia kwa kiasi kikubwa kukiukwa kwa sheria za kazi, ikiwemo kutolipwa stahili zinazokidhi mahitaji, kukosa mikataba ya kazi na mazingira duni ya kufanyia kazi.
 Shua Ndereka kutoka redio OKOA alisema kutokana na kukosekana kwa chama cha wafanyakazi kwa vyombo vya habari kumechangia idadi kubwa waandishi kulipwa maslahi duni na kuafanyakazi katika mazingira duni.
 “Wanahabari wamekuwa mbele kupigania maslahi ya wengine huku wenyewe wakishindwa kujipigania na hili limechangiwa na kutokuwepo kwa chama cha wafanyakazi, hivyo ujio wa JOWUTA utasaidia kuwawezesha wafanyakazi wa sekta ya habari kuwa na maslahi bora iwapo kitatimiza majukumu yake ipasavyo,” anasema.
 Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya JOWUTA na mshauri wa masuala ya habari Samson Kamalamo ameeleza kuwa chama hicho kitasiammia owuta kitasimamia sheria katika kutimiza majukumu yake pasipokuegemea upande wowote.

 Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja Mara baada ya kukabidhiwa vteti vyao.


 Alisema pamoja na lengo la chama hicho kutetea maslahi ya wafanyakazi wa sekta ya habari lakini pia kitasisitiza uwajikabi wenye tija na weledi na kwamba haitawaunga mkono waandishi wa habari wanaokiuka sheria.
 Kamalamo alisema ni vyema waandishi wa habari wakajiendeleza kielimu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
 “Sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 inamtaka mwandishi ifikapo mwaka 2022 waandishi wawe na elimu kuanzia ngazi ya diploma sasa wale wenye ngazi ya cheti wanatakribani miaka minne mbele wawe wameshatoka hapo vinginevyo hatutakuwa nao,”alisema Kamalamo.
 Naye Katibu wa chama hicho Timothy Kitundu alisema JOWUTA imekamilisha taratibu zote za kupata usajili ikiwemo kuandaa katiba, kanuni na kulipia gharama za usajili.
Alisema chama hicho tayari chama hicho kimeendesha mafunzo ya masuala ya usawa jinsia na kufanyakazi katika maeneo na mazingira hatarishi kwa zaidi ya waandishi wa habari 60 katika mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro.
 source:Maua MagonaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.