Thursday, August 22

Urusi noma! Yatimua wanadiplomasia kutoka nchi 23

0
MOSCOW, Urusi
BAADA ya wanadiplomasia wake kutimuliwa kutoka mataifa ya Ulaya, Urusi nayo imetangaza kutimua wanadpiplomasia kutoka nchi 23, ikiwa ni kitendo cha kulipiza kisasi huku ikiitaka Uingereza kupunguza watu wake kufikia idadi iliyobakizwa na Urusi nchini humo katika kipindi cha mwezi mmoja.
Aidha ubalozi mdogo wa Marekani uliopo St. Petersburg  nchini Urusi umefungwa baada ya wanadiplomasia 60 waliopo katika ubalozi huo kutimuliwa.
Msuguano uliopo umesababishwa na maofisa ubalozi wa Urusi kutimuliwa katika nchi hizo kufuatia madai ya Uingereza kwamba, Urusi ilihusika katika kumtilia sumu jasusi (mwenye ngozi mbili) Sergei Skripal na binti yake.
Mapema mwezi huu nchi zaidi ya dazeni ziliiamuru urusi kupunguza wanadiplomasia wake kupinga kile walichodai kutiliwa sumu kw ajasusi huyo ambaye alikuwa anahifadhiwa na Uingereza huko Salisbury , Machi  4.
Kwa mujibu wa taarifa nchi zinazohusika na sheshe hilo ni  Australia, Albania, Ujerumani, Denmark, Ireland, Hispania, Italia, Canada, Latvia, Lithuania, Macedonia, Moldova, Uholanzi, Norway, Poland, Romania, Ukraine, Finland, Ufaransa, Croatia, jamhuri ya Czech, Sweden na Estonia.
Nchi nyingine ambazo zitaingizwa ni Ubelgiji, Hungary, Georgia na  Montenegro.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.