Thursday, August 22

TANTRADE-SIMIYU KUSHIRIKIANA NANENANE KITAIFA

0
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) watashirikiana kwa pamoja kuandaa Maonesho ya Kilimo NaneNane Kitaifa  yatakayofanyika Mkoa wa Simiyu Mwaka 2018.
Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa utatoa dira ya kuyafanya Maonesho ya Kilimo NaneNane yawe ni Maonesho ya Kilimo Biashara ili Watanzania wapate fursa ya kuona teknolojia mbalimbali kwenye eneo la kilimo, mifugo na uvuvi.
 
“Matarajio yetu kama mkoa kwa kushirikiana na TanTrade ni kuona kwamba tunaingiza Maonesho ya Kilimo NaneNane kuwa tukio ambalo litawakaribisha watu wenye teknolojia mbalimbali Kitaifa na Kimataifa kwenye kuwezesha mageuzi ya kilimo,uvuvi na ufugaji wa nchi kwa kuonesha ni kwa namna gani wanaweza kumfikia mkulima, mvuvi na mfugaji mdogomdogo kwenye teknolojia ya kisasa ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi ili Maonesho ya Kilimo NaneNane yawekwe kwenye ramani ya dunia” alieleza Mhe Mtaka
Aliendelea kwa kuziomba Balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali kuyatumia Maonesho haya kuyatangaza kwa kukaribisha makampuni yenye teknolojia kuja kuonesha mkoani Simiyu. Na Mhe Mtaka alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kwa makundi yote kutoka ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika eneo litakalofanyika Maonesho ya Kilimo Biashara ili uwekezaji huo uendane na viwango vya Kimataifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw. Edwin Rutageruka ameeleza kuwa TanTrade ni taasisi pekee iliyopewa jukumu la kusimamia masuala ya Maonesho ndani na nje ya nchi kisheria.
Hivyo, Bw Rutageruka amesema kutokana na uzoefu wa uandaaji wa Maonesho mbalimbali,  kwa mwaka 2018 Maonesho ya Kilimo Biashara yatakuwa ni Maonesho bora kwasababu watawaandaa washiriki wote Kisekta,  kuweka miundo mbinu ya kisasa na kuyafanya Maonesho haya kuwa ya Kimataifa.
“Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ina kiu ya kuona Maonesho ya Kilimo Biashara  yanakuwa ya kisasa  kama ilivyo Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambayo kwa Afrika Mashariki ndio Maonesho yanayoongoza kwa ubora na Maonesho haya ya Kilimo tutayafikisha huko” aliongeza Bw Rutageruka
Imetolewa na
KITENGO CHA MAWASILIANO-TanTrade
                        Read More

Share.

About Author

Comments are closed.