Wednesday, August 21

Sharon Stone ndani ya bikini na bonge la pete

0
YULE mkali wa sinema ya  Basic Instinct amedhhirisha kwamba katika mapenzi umri ni namba tu lakini mambo yako bambam. Mdada huyu ambaye Machi 10 mwaka huu ametimiza miaka 60 ameonekana kitamba na  bikini na pete n zito ya almasi mkononi huku akitatarika na  mtu ambaye hajulikani sana katika mazingira ya mapenzi.

Swali kubwa ambalo lipo kwa watu na hasa wapenzi wake je  amechumbiwa katika umri wake huo?Stone,ambaye alishawahi kuolewa na o Michael Greenburg kutoka mwaka 1984 hadi 1990 na Phil Bronstein kuanzia 1998 hadi 2005, alionwa na pete  yenye kito cha almasi katika mkono wake huku akiwa na mtu ambaye hakuwa anajulikana wakishikanashikana katika fukwe.
Katika skuhikana shikana huko kulifanywa na hao wawili ambao Januari mwaka huu walionwa pamoja kwa mara ya kwanza.
Stone ambaye anajulikana kama Hot Mama katika mizunguko ya Ulaya ana watoto watatu na wote hao ni wa kuasili. Yupo Roan Joseph Bronstein, 17, anayeshea na mume wake wa zamani na pia ni mama wa Laird Vonne Stone, 12, na Quinn Kelly Stone, 11.

Read More

Share.

About Author

Comments are closed.