Thursday, August 22

RPC Mkumbo apigania maisha

0
KAMANDA wa polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo amepata ajali jana eneo la Mdori mkoani Manyara wakati akisafiri kutoka mkoani Singida kuelekea Jijini Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Polisi mkoani Arusha, hali ya Kamanda Mkumbo siyo nzuri na yuko katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.
Imeelezwa kuwa amepata majeraha makubwa kichwani.
Akizungumza jana jijini Arusha, Msemaji wa Jeshi la Polisi mkoani hapo, Rashid Mohamed alikiri Kamanda huyo kupata ajali akiwa na gari yake ya kazi aina ya Toyoto Land Crusser yenye namba za usajili PT 2040.
Mganga Mfawidhi wa hospital hiyo, Omary Chande alikiri kumpokea kamanda huyo ila alisema hawezi kusema chochote kwa kuwa alikuwa kwenye chumba cha upasuaji akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa chanzo cha ajali ilikuwa ni kupasuka kwa tairi mbili, moja ya mbele na nyuma na kupinduka zaidi ya mara mbili.
 Dereva wa gari hilo, Sajenti Silvanus na mlinzi wa Kamanda Mkumbo, Konstebo Magenda wako salama salmini na hawakuwa na majeraha yoyote mara baada ya kutokea ajali hiyo, majira ya Saa 9:30 alasiri.

Source:HabariLeoRead More

Share.

About Author

Comments are closed.