Monday, August 19

Rasimu vibanda vya kuonesha filamu kukamilika Mei

0


RASIMU ya kwanza kuhusiana vibanda  vya kuonesha filamu inatarajiwa kukamilika Mei mosi  na itajadiliwa na wizara ya Habari ,utamaduni ,sanaa na michezo  kabla ya kupelekwa kwa wadau ili nao waeleze maoni yao.
Mambo hayo yanafanyika ili kutekeleza sheria ya filamu ya mwaka 1976 na kanuni zake za mwaka 2011 zinazotambua miundombinu ya filamu na maeneo ya kuonyesha kama moja ya fursa  ya kutanua wigo wa solo na wadau kuonyesha kazi zao.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu mtendaji bodi ya filamu Tanzania Joyce Fissoo katika semina iliyowakutanisha wadau wa filamu na michezo ya kuigiza .
Alisema serikali kupitia wizara ya Habari ,utamaduni ,sanaa na michezo ,kamati ya bunge ya huduma za jamii imeielekeza bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kutengeneza kanuni mahususi kwa ajili ya vibanda vya kuonyesha filamu ili viweze kuwa na fursa  ya soko na manufaa .
Alisema kanuni hizo zitasaidia kwani kumekuwa na changamoto  katika baadhi ya  vibanda vinavyoonyesha filamu kutokuwa katika hali nzuri ambayo ni hatarishi kwa maisha ya watu katika kazi zao.
” Tunashukuru Arusha wametupa maoni na michango juu ya mini cha kuzingatia kwenye kanuni mpya itakayoundwa kwani Wizara utamaduni wake ni kuhakikisha inapotengeneza nyaraka itakuwa ni nyaraka shirikishi sababu watekelezaji wake ni  wananchi,”alisema Fissoo.
Aidha Fissoo alisema Bodi ya filamu ina mikakati ya kuboresha filamu za ndani ili kuhakikisha zinakuwa na soko bora la ndani na nje ya nchi na hii itachangiwa na kuwajengea uwezo wadau wa filamu ili waweze kuzalisha kazi zenye Ubora. 
Naye ofisa utamaduni Mkoa wa Arusha Irene Ngao aliwasihi wasanii kuwa na umoja ili waweze kutengeneza kazi ambazo zitakuwa na ubora wa hali ya juu pia wasanii waweze kuwasilisha kazi zao katika bodi za gilamu za wilaya na mkoa ili ziboreshwe zaidi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.