Sunday, August 25

NEC yatangaza nafasi za ajira za muda za uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura

0


<br /> NEC yatangaza nafasi za ajira za muda za uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura | Lukwangule Entertainment<br />

Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi za kazi za muda kwa ajili ya Uboreshaji wa
Daftari la Wapiga Kura.
Kwa mujibu wa
tangazo la maombi ya ajira hizo lililosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi
Mabamba Rajabu Moses, Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na wasiozidi miaka
45 wametakiwa kuomba.
Kwa mujibu wa
tangazo hilo, sifa zingine za waombaji ni kuwa na elimu ya kidato cha nne na
kuendelea na awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
“Awe  na
uwezo wa kutambua matatizo ya kompyuta ya hardware na software an kuyatatua”
ilisema sehemu ya tangazo hilo na kuongeza kuwa:.
“Awe na uwezo wa
ku-istall programu za kompyuta an kutoa msaada wa kuifundi wa TEHAMA kwa
watumiaji.”
“Awe hajawahi
kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai an awe na uwezo wa kufanya kazi katika
mazingira yenye usimamizi mdogo”
Sifa nyingine za
ziada za kazi hiyo zimetajwa  kwenye tangazo hilo linalopatikana kwenye
Tovuti ya NEC ya www.nec.go.tz na mitandao ya kijamii ya NEC.

 

Share.

About Author

Leave A Reply