Sunday, August 18

Moruwasa wataka ushirikiano kuboresha huduma za maji

0

Akizungumza na blog ya Lukwangule ofisini kwake Afisa Habari wa mamlaka hiyo Getrude Salema alisema MORUWASA imedhamiria kuwapa wananchi huduma bora na kwamba nao wana wajibu wa kutoa taarifa pindi wanapokuwa na matatizo ili yaweze kupatiwa ufumbuzi.
Kauli ya Salema inafuatia malalamiko ya baadhi ya wananchi wa manispaa ya Morogoro kudai kwamba utaratibu wa mgao wa maji ulipangwa na mamlaka hiyo unakiukwa.
Alibainisha kuwa, ili MORUWASA iweze kutatua changamoto za zinazowakabili wananchi hawana budi kuziwasilisha katika mamlaka hiyo ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Baadhi ya wananchi walioongea na Lukwangule walidai kuwa, katika baadhi ya maeneo huduma ya maji inakosekana hadi kufikia siku tano jambo ambalo linawaathiri.
Mmoja wa wananchi hao Habiba Sompa mkazi wa Kihonda katika manispaa hiyo alisema huduma ya maji katika eneo hilo kwa sasa imekuwa ya kusuasua tofauti na ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.
Alisema hapo nyuma walikuwa wakipata maji kila baada ya siku moja lakini kwa sasa maji wanaweza kukaa hata wiki moja bila ya huduma ya maji.
Sompa alisema hata pale yanapotoka maji hayo hutoka nyakati za usiku hivyo kwa wananchi ambao hawajaunganisha mabomba katika nyumba zao hujikuta wakipata tabu.
“Nyumba ninayoishi  hatuna bomba tunachangia bili kwa jirani shida tunapata maji yakitoka usiku wenye nyumba hawafungui mlango mpaka wakinge wao sasa tukianza kukinga sie kabla hatujamaliza yamekatika ,” alisema Habiba.
Kwa upande wake Sylvia Samwel wa Kihonda kilombero  alisema kuwa kwa sasa wameshazoea kuyaona maji baada ya siku tano nakuendelea  na taarifa walishatoa kwa wasoma mita japo si rasmi kama kufika ofisini.
Alisema kuwa ni vyema Moruwasa wakafata ratiba waliyojiwekea ili kupisha usumbufu wanaopata wananchi kusubili maji hadi nyakati za usiku na wakati mwingine hata usiku hawayapati.
Alieleza kuwa iwapo Moruwasa itafata ratiba iliyoweka kila baada ya siku moja tatizo la maji litakwisha hivyo ni vyema wakafata ratiba ili kutatua tatizo hilo.
“Kinachoudhi maji hatupati kwa wakati ikija bili tunachajiwa na service charge iko pale pale ona sasa ukisoma bili maji tuliyotumia ghalama ndogo kuliko hata service charge alisema Sylvia.
Asifa habari Salema  alieleza kuwa Moruwasa ina aina mbili za mgao wa maji ambao umegawa mjini na kihonda ambapo maji yakitoka mjini kihonda hayatoki  siku nzima hivyo hivyo kwa mjini.
Aidha amefafanua kuwa mgao mgao wa pili ni wazaidi ya siku moja hivyo maji yanaweza yatoka zaidi ya siku moja na kutotoka zaidi ya siku moja.
Mamlaka ya majisafi na majitaka manispaa ya Morogoro imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupanuka kwa mji kunakochangia ongezeka la idadi ya watu.
Source:Maua Magona Read More

Share.

About Author

Comments are closed.