Monday, August 19

Magufuli aiibua keko Phamaceticauls, atoa somo kwa wizara

0
RAIS Dk. John Magufuli amehimiza wafanyabiashara na wawekezaji kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba.
Akizungumza katika uzinduzi wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) yatakayotumika katika usambazaji wa dawa na vifaa tiba nchini, Rais Magufuli alisema licha ya kiasi kikubwa cha fedha zinazotengwa na serikali kwa ajili ya kununua dawa ni kiasi kidogo tu ndicho kinachobaki nchini.
Alisema katika kiasi kinachofikia shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kununua dawa, ni asilimia sita tu ndiyo ya dawa ndizo zinanunuliwa hapa nchini na kiasi kinachobaki kinaagizwa kutoka nje.
Rais Magufuli alisema kama kungekuwa na viwanda vingi vya kuzalisha dawa  fedha hizo zingeweza kubaki nchini na kuzalisha ajira kwa watanzania.
“Sekta ya afya ni nyeti bila kuimarishwa ni ndoto kupata maendeleo. Tunahitaji wananchi wenye afya njema ili kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda,” anasema.
Alieleza kuwa, “nchi ina changamoto nyingi tushirikiane kuondoa kero za wananchi, tunahitaji kujenga Viwanda vya dawa kwa sababu”.
Rais Magufuli alisema ni aibu kwa nchi kuona fedha nyingi zinazotengwa kwa ajili ya kununua dawa zikienda nje ambapo aliitaka Wizara ya afya kuangalia uwezekano wa kuweka utaratibu ambao utawawezesha wazawa kupata mitaji ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli aligusia kuhusu utendaji wa kiwanda cha dawa cha Keko Pharmaceticauls na kwamba kama ubia huo umeshindwa kuwa na faida ni vyema wizara ya afya iangalie uwezekano wa kununua hisa za mwekezaji ili kiwanda hicho kiendeshwe na serikali.
“Pengine tulikosea maana tumeingia ubia TTCL tumeshindwa, tumeingia katika reli tumeshindwa tukaamua kununua hisa sasa tunajenga reli wenyewe, wizara liangalieni hili,” Rais Magufuli alieleza.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurian Bwanakulu alisema taasisi hiyo ipo katika mchakato wa kutanza zabuni kwa ajili ya kwa ajli ya kuwaita sekta binafsi wanaotaka kuwekeza katika viwada vya dawa.
Aisema MSD imeingia mkataba na viwanda 199 vya kuzalisha dawa ambapo kati ya hivyo viwanda vya ndani ni 14 ambavyo hupata shilingi bilioni 28 sawa na asilimia sita ya fedha za kununua dawa kiasi kinachofikia shilingi bilioni 500.
Akizungumzia magari hayo Bwanakulu alisema yatasaidia kupunguza muda wa MSD kupeleka dawa katika vituo vya tiba kutoka miezi mitatu hadi miwili, lakini pia itaokoa zaidi ya shilingi milioni 500 kwa ajili ya usafirishaji wa dawa na kupunguza gharama ya uhifadhi wa dawa.
Kwa upande wake Waziri wa afya Ummy Mwalimu alisema serikali imeendelea kuongeza bajeti ya Wizara ya Afya ili kuboresha huduma za tiba ambapo katika mwaka wa fedha 2017/18 ilitenga shilingi trilioni mbili.
Alifafanua kuongezeka kwa bajeti ya sekta ya afya kumesaidia kuboresha huduma za afya ambapo alitolea mfano kuanza kwa huduma ya kupandikiza figo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Benjamin Mkapa mkoani Dodoma.
Waziri Mwalimu alieleza kuwa, uboreshaji wa huduma za afya pia umepunguza idadai ya wagonjwa wa moyo wanaokwenda kupatiwa matibabu nje ya nchi.
Source: Said MmangaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.