Monday, August 19

Kutana na DJ Wika, DJ mzee kabisa wa miaka 80 anayewapeleka mbio vijana

0
Akiwa na miaka 80 Wirginia Szmyt bado anabamiza katika nafasi yake ya kuchezesha muziki (DJ) huko Hulakula mjini Warsaw, Poland.


Wirginia Szmyt, ambaye pia anajulikama kama DJ Wika, anajulikana vyema nchini Poland kama DJ mzee kabisa ambaye bado analiendesha libeneke pamoja na kwamba ana miaka 80.

Ajuza huyo aliyezaliwa mwaka 1938 sasa ni DJ na amekuwa akicheza muziki katika radio na pia katika hafla mbalimbali anazoalikwa.DJ Wika kwa miaka yake yote jinsi anavyowapeleka krezi wapenzi wa muziki, anafanya vyema zaidi kuliko vijana ambao wanajiona kwamba wanajua kupeleka ngoma  zenye nakshi kwa wasikilizaji wao.Ajuza huyu anasema kwamba ni vyema watu  wakafanya yenye kufurahisha nafsi ili kufa kwa furaha wakifurahia maisha badala ya kujiogopa wanavyozeeka.Wirginia amekuwa akispin salsa, rumba, na trak za disko  kwa wazee kama yeye, vijana na vijana wa kati.

Anasema alipoanza kuwa DJ alikuwa na shughuli nyingi za kufanya kama utafutaji wa wimbo katika CD kaseti mpaka kuirudiosha unapotaka na mashine lakini kwa sasa mambo yamerahisishwa kutokana na uwapo wa kompyuta.Anasema ingawa miziki yote ni mizuri yeye huwa hapendi sauti kubwa ya spika kwani inashindwa kumpa mtu ladha ya mdundo wa kueleweka, ingawa anajua wanachopenda vijana lazima uwape.


Anasema yeye anafurahi jinsi anavyowafanya watu wafurahi anapochezesha muziki na kwamba hajali jinsi  alivyochelewa kuwa DJ.

DJ Wika hugonga mara mbili muziki wake kwa watu wazima katika klabu ya Bolek Club mjini Warsaw, Poland na kutandaza utaalamu wake kila siku katika radio.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.