Monday, August 19

Hekaheka anga za juu, kituo cha China kinaporomoka kwa kasi

0
KITUO cha anga za juu  cha taifa la China tiangong-1 kimegeuka tishio kwa uhai duniani kufuatia kutojulikana kitaangukia wapi wakati kikirejea duniani kwa kishindo kufuatia mifumo yake ya udhibiti kushindwa kufanyakazi.
Kituo hicho cha kwanza kutengenezwa na taifa hilo ambalo limepiga hatua kubwa ya maendeleo, kinarejea duniani na kasi ya maili 17,000 kwa saa.
Wataalamu wa sayansi wanasema kwa kasi hiyo kinatarajiw akuanguka duniani mwishoni mwa wiki ambapo ni siku za Pasaka.
Pamoja na mwendo wake kubainika kuingia dunia mwishoni mwa wiki bado wataalamu hawajajua wapi itaangukia.
Tiangong-1, au “Kasri la Mbingu,” litajulikana linaangukia wapi mara tu baada ya  kupita ukanda mgumu  na hivyo kutoa muda mfupi sana kwa kuokoa wananchi kama litakuwa linangukia mjini au katika makazi ya watu.
Kituo hicho chenye uzito wa tan inane kilitakiwa kitua duniani kwa kudhibitiwa, na eneo lake likuwa ni kwenye kina kikuu chya bahari ya Pacific kilomita kadhaa kutoka katika makazi ya watu.
Lakini Machi mwaka jana, China  ilipoteza mawasiliano na kituo hicho na wanasayansi wa China wakashindwa kuwasha injini zake kubadili mwelekeo ili kukipa mwelekeo mpya.
Imeelezwa kuwa kuanzia wakati huo chombo hicho kimekuwa kikishuka katika mazingira ya hatari. Jumanne wiki hii chombo hicho kilibainika kuwa katika umbali wa maili 130, kikianguka kwa kasi sana kuliko ilivyokuwa awali.
Imeelezwa kuwa kituo hicho kitaingia katika kano ya dunia kati ya Machi 31 na Aprili 4.
nchi zilizo hatarini

Pamoja na wanasayansi wa China kusema kwamba kituo hicho kitaungua na kumalizika wakati wakipita kano hiyo, wataalamu wengine wanasema kwa ukubwa wa chombo hicho asilimia 10 hadi 40 ya chombo hicho kitaweza kupita na kwamba mabaki yake yataangukia baharini au katika nchi kavu kwenye makazi ya watu.
Msemaji wa Taasisi ya utafiti wa anga za juu ya Ulaya (ESA) amesema: “Unaweza kuwa na uhakika kabisa kwamba Tiangong-1 itasambaratika wakati wa kupita katika kano, na  baadhi ya mabaki yatafika duniani.”
Kituo hicho kilirushwa angani Septemba 2011 na  kilikuwa na lengo la kujaribu teknolojia za utuaji katika uzio wa duniakatika anga za juu.
China imetoa taarifa kidogo sana kuhusiana na kituo hicho ikieleza zaidi umbali bila kutoa taarifa ya muundo wake na Shirika la utafitio wa anga za Juu la Marekani (NASA) lina taarifa chache zaidi za kuwezesha kubashiri mahali ambapo litaangukia.
Rais  Xi Jinping, amekuwa akitaka taifa lake kuwa taifa kubwa katika masuala ya anga za juu huku wakiimarisha ulinzi na usalama wa taifa hilo.
Tiangong-1 ilikusudiwa kuondolewa kazini mwaka 2013 lakini China imekuwa ikiahirisha tukio hilo na kuendelea kuipigisha mzigo.
Kwa sasa imeelezwa na wataalamu kwamba kituo hicho kinaporomoka kila baada ya dakika tatu wakati ikipiga mbio mara 16 kuzunguka dunia kwa siku.
Hata hivyo baadhi ya wataalamu wamekuwa wakisema kwamba uwezekano wa kuleta madhara kwa wanadamu ni mdogo.
Stijn Lemmens, wa ESA mtaalamu wa mabaki ya anga za juu mwenye makazi Ujerumani anasema: ” katika kipindi cha miaka 60 za usafiri wa anga zikiwemo anga za juu tumefikia mahali tuna vyombo takribani 6000 visivyodhibitiwa vinapasua kano na kuanguka duniani hasa setelaiti na mifumo ya maroketi inayotuma vyombo anga za juu.
“Ni katika tukio moja tu mabaki yaliweza kumpiga mtu lakini hakuna majeruhi.”
Anasem,a uwezekano wa kupigw ana mabaki ni moja kwa trilioni 1.2  au mara  milioni 10 million kama kupigwa na radi.
Mtu anayejulikana kupigwa na mabaki ya vyombo vya anga za juu ni Lottie Williams, wa Tulsa, Oklahoma.
Mwaka  1997 alipigwa na kipande cha chuma cha inchi sita kilichodndoka kutoka katika roketi la  Delta 2 .Read More

Share.

About Author

Comments are closed.