Thursday, August 22

Akina Mbowe na wenzake wapata dhamana, rasmi Jumanne

0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewapatia dhamana viongozi sita wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe bila wao kuwapo mahakamani.
Hata hivyo wataendelea kuwapo mahabusu ya Segerea hadi Aprili 3, mwaka huu, ili waweze kupatiwa dhamana rasmi ikiwa ni pamoja na kuwathibitisha wadhamini kwa kusaini nyaraka za mahakama.
Mbali na Mbowe, washitakiwa wengine ni Katibu wa Chama hicho, Dk Vicent Mashinji, Naibu Katibu mkuu wa Chadema upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko.
Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka nane ya kufanya mkusanyiko usiohalali uliosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwilina Baftaa na uchochezi wa uasi.
Kabla ya kusomwa uamuzi huo, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alihoji sababu za kutokuwepo kwa washitakiwa hao ambapo ofisa wa magereza, Inspekta Shaban aliieleza mahakama hiyo kuwa gari ambalo walipanda washitakiwa wote kutoka gereza la Segerea hawakuweza kufika mahakamani hapo kwa kuwa walipofika njiani lilipata hitilafu na kuharibika.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.