Sunday, August 25

Michezo Plus

0


Klabu ya Ujerumani EINTRACHT FRANKFURT imemsajili rasmi mshambuliaji mwenye umri wa miaka 18 raia wa Cameroon, mwenye jina sawa na Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliefariki mwaka 2013.

 

Nelson Mandela Mbouhom alianza kusakata kabumbu kwenye mji wa Barcelona, kabla ya kuondoka La Masia akiwa na umri wa miaka 13 na kuelekea Ujerumani.

Mwaka mmoja baada ya kujiunga na Hoffenheim’s academy, Mandela alihamia kwenye klabu ya vijana ya Frankfurt. Nyota huyo amefunga jumla ya mabao nane katika mechi 14 alizocheza.

Msimu uliopita klabu ya Frankfurt ilishika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi ya Bundasiliga, meneja Niko Kovac anatarajia nyota huyo atakuwa na hekima, malengo na mafanikio kama wajina wake.

The post NELSON MANDELA ASAINI MKATABA RASMI NA CLUB YA EINTRACHT FRANKFURT HUKO UJERUMANI. appeared first on Michezo Plus.Read More

Share.

About Author

Leave A Reply