Thursday, August 22

WAZIRI WA NISHATI DR. MEDARD KALEMANI (MB) AIPA TANESCO MIEZI 3 KUHAKIKISHA MITA ZA UMEME ZINANUNULIWA KWA WAZALISHAJI WA NDANI

0


Waziri wa Nishati,Dk Medard Kalemani akipata maelezo kutoka kwa Mkurungezi mkuu wa Baobab  Energy Systems  Tanzania Injinia Hashim Ibrahim kuhusu namna ya mita za umeme zinavyotengenezwa,alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Goba,Dar es Salaam Mapema jana.

Waziri wa Nishati,Dk Medard Kalemani (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa  Baobab  Energy Systems  Tanzania kuhusu namna ya mita za umeme zinavyotengenezwa,alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Goba,Dar es Salaam Mapema jana.

Waziri wa Nishati,Dk Medard Kalemani akiwa katika picha ya pamoja na  Mkurugenzi mkuu wa Baobab  Energy Systems  Tanzania Injinia Hashim Ibrahim na wafanyakazi wa kiwanda hicho alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Goba,Dar es Salaam Mapema jana.
Waziri wizara ya Nishati Dk Medard Kalemani (MB), jana alitembelea kiwanda kipya cha kutengeneza mita za umeme kiitwacho Baobab  Energy Sytems Tanzania, kilichopo eneo la Mbezi Juu jijini Dar es salaam,kiwanda hiki  kinamilikiwa na watanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mheshimiwa Waziri amesifu uwekezaji uliofanywa na watanzania hawa, na kueleza wazi kwamba hiki ni kiwanda cha kwanza chenye teknolojia chanya inayolenga kusaidia Tanzania kuokoa gharama za manunuzi ya mita na vifaa vya umeme kutoka nje ya nchi.

Katika maelezo yake, Mheshimiwa Dr Kalemani(MB) ameipa Tanesco miezi 3 kuhakikisha wanasitisha ununuzi wa mita za umeme kutoka nje ya nchi kwani tayari viwanda vya ndani kikiwamo Baobab  vimeonesha kuwa na uwezo wa kuzalisha kukidhi mahitaji ya nchi.
 “Kwa sasa kiwanda kinauwezo wa kuzalisha mita za umeme elfu thelathini na nane(38000) kwa mwezi, wakati mahitaji ya Tanesco ni mita elfu ishirini kwa mwezi (20000), hivyo naipa tanesco miezi mitatu waangalie kazi inayofanywa na wataalamu hawa na waanze kununua mita hizo kutoka kwa wazalishaji hawa wa ndani”.
 Kwa sasa nchini Tanzania kuna viwanda viwili vya uzalishaji wa mita za umeme, Baobab  ikiwa ni kiwanda kimoja wapo.
Pia Mheshimiwa Waziri ameiagiza tanesco kushirikiana na wazalishaji hawa wa mita za umeme ili kupunguza ulazima wa kupeleka mita na vifaa kama hivi nje ya nchi kwaajili ya matengenezo pindi vinapo haribika.
Akiendelea kufafanua Injinia Hashim Ibrahim amesema kwamba wamewekeza katika uzalishaji huu wa mita za umeme, kwani wameona changamoto kubwa serikali inayopata kuagiza mita kutoka nchi nyingine, jambo ambalo linapelekea uhaba wa Mita hizi zinazozalishwa nchini zina ubora wa kipekee unaoweza kutambua mwizi wa umeme, upotevu wa umeme na pia zinapatkana kwa gharama nafuu zaidi ukilinganisha na gharama ambazo kwa sasa zinatumika kununua mita hizi.

Injinia Ibrahim ameahidi kwamba kiwanda hichi kimelenga kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania hasa wanaohitimu vyuo mbalimbali hapa nchini vikiwamo Veta.

Pia ameeleza kwamba malengo mapana ya uanzishaji wa kiwanda hichi pia ni kusaidia jitihada za mheshimiwa rais wa awamu ya tano Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwenye sera yake ya uwekezaji wa viwanda.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.