Thursday, August 22

Utafiti:Ulaji Mikate,Keki Na Vingine Vya Kusindikwa Huleta Saratani

0


Utafiti mpya uliofanywa na Watafiti nchini Ufaransa wanasema kuna uhusiano kati ya vyakula vilivyosindikwa na maradhi ya saratani.
Kwa mujibu wa  watafiti hao wameainisha vyakula ikiwemo keki,kuku na mikate kuwa vinasindikwa sana.
Utafiti huo  ulifanywa kwa watu 105,000 umeonyesha kuwa vyakula hivyo huliwa zaidi, hivyo wako hatarini kupata saratani.
Wanasayansi kutoka chuo kikuu Sorbonne jijini Paris walifanya utafiti kufahamu vyakula ambavyo watu hupendelea kula, ambapo Wanawake wa makamo walikuwa wakifuatiliwa kwa miaka mitano
Matokeo kutoka jarida la kitabibu la nchini Uingereza yanaonyesha kuwa ikiwa kiasi cha vyakula vilivyo sindikwa sana vitaongezeka kwenye mlo kwa 10% basi idadi ya ongezeko la ugonjwa litafikia 12%.
Tahadhari nyingi zimetolewa lakini wataalamu wanasema kuzingatia lishe bora ni bora zaidi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.