Friday, April 19

Ushindi wa Simba SC dhidi ya Al Ahly wamuibua Rais wa TFF

0


Ushindi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameipongeza Simba SC kwa ushindi walioupta dhidi ya Al Ahly.

Licha ya pongezi hizo, Karia amesema kuwa wao kama Shirikisho ni kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega kwa timu zinazowakilisha nchi kimataifa ili zifanye vizuri.

“Nawapongea Simba wamefanya vizuri, sisi kama TFF jukumu letu ni kuzipa sapoti timu zote zinazowakilisha nchi, hivyo wengine wanapaswa kupambana ili waipe uwakilishi mzuri Tanzania,” amesema Karia.

Hapo jana wekundu wa Msimbazi, Simba SC katika dimba la Uwanja wa Taifa Dar es Salaam waliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Al Ahly kutoka Misri na kuwafanya kufikisha pointi 6 katika kundi lao.

Share.

About Author

Leave A Reply