Thursday, August 22

TP Mazembe yamfukuzia Kichuya “La Pulga” kimya kimya

0Baada ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kirafiki baina ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya DR Congo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Shiza Ramadhani Kichuya “La Pulga” inadaiwa mchezaji huyo kuwindwa na TP Mazembe.
Duru za habari zinasema kuwa mabosi wa klabu ya TP Mazembe ya Congo wanajipanga kutua nchini kufanya mazungumzo na vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC kwaajili ya kumnasa Kichuya ambaye hivi karibuni amepata jina la utani la Messi “La Pulga”  kutoka kwa msemaji wa timu hiyo, Haji Manara.
Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe la hapa nyumbani limeandika kuwa rafiki wa karibu wa meneja wa mchezaji huyo, Profesa Madundo Mtambo ameliambia kuwa kwa sasa hawazingatii maslahi pekee bali ni kutaka kuona Kichuya anapata nafasi ya kubadili mazingira na kurejea tena nchini kuitumikia Taifa Stars akiwa na mbinu zaidi.
Shiza Kichuya ambaye alipachika bao la pili kwenye mchezo huo dhidi ya DR Congo baada ya Samatta kufunga la kwanza mkataba wake unatarajia kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu wakati amejiunga na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.