Thursday, August 22

TANZIA: Muigizaji wa kwanza wa kike kupata umaarufu Bollywood, Afariki dunia

0


Muigizaji wa kwanza wa kike kupata umaarufu zaidi kwenye soko la filamu nchini India (Bollywood), Sridevi Kapoor jana usiku amefariki dunia kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na miaka 54.
Tokeo la picha la Sridevi Kapoor

Sridevi Kapoor
Taarifa iliyotolewa na familia yake imesema Sridevi alikuwa na familia yake mjini Dubai kuhudhuria harusi wa mpwa wake.
Sridevi amekuwa kwenye tasnia ya filamu kwa miongo minne ambapo amefanikiwa kushiriki kwenye filamu 300 na baadhi ya filamu zilizompa umaarufu ni kama Mr. India, Chandni, ChaalBaaz na Sadma.
Sridevi alitajwa kuwa mmoja wa wasanii wachache wa kike waliopata mafanikio makubwa bila ya msaada wa wanaume.
Baada ya taarifa hizo, maelfu ya watu walikusanyika nje ya nyumba yake jijini Mumbai huku  waigizaji wenzake na viongozi wa serikalini akiwemo Rais wa India Ram Nath Kovind kupitia ukurasa wake wa Twitter akiandika “Shocked to hear of passing of movie star Sridevi. She has left millions of fans heartbroken. Her performances in films such as ‘Moondram Pirai’, ‘Lamhe’ and ‘English Vinglish’ remain an inspiration for other actors. My condolences to her family and close associates,”
Naye Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ameandika katika mtandao wa twitter “Saddened by the untimely demise of noted actor Sridevi. She was a veteran of the film industry, whose long career included diverse roles and memorable performances. My thoughts are with her family and admirers in this hour of grief. May her soul rest in peace.”
Kifo cha  Sridevi kinakuja ikiwa ni miezi miwili imepita tangu mjomba wake ambaye alikuwa ni moja ya waigizaji nguli wa filamu nchini humo, Shashi Kapoor aage dunia.
CHANZO;BONGO5Read More

Share.

About Author

Comments are closed.