Saturday, August 17

Sirocco: Nokia yaunda simu imara zaidi duniani ya Android

0


Nokia phones
Kampuni ya Nokia imetangaza kuwa imeunda simu ya Android ambayo ndiyo imara zaidi kiasi kwamba haiwezi kuvunjwa kwa mkono.
Kampuni hiyo pia imeanza kuuza simu nyingine yenye sehemu ya kuteleza, ambayo inafanana na simu zilizokuwa maarufu mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Simu hiyo ya Nokia 8 Sirocco imeundwa kwa sehemu ya juu ya chuma cha pua na inadaiwa kuwa imara zaidi kwa sasa.
Simu ya Nokia 8110 inakumbatia muundo wa zamani wa simu, ambao ulitumiwa kwenye filamu za Matrix.
Wachanganuzi wanasema simu hizo mbili zitaendeleza ufanisi wa simu za Nokia sokoni uliopatikana mwaka jana kutokana na uuzaji wa simu maarufu za zamani za Nokia 3310.
Ingawa simu hizo zinauzwa kwa jina la Nokia, zinaundwa na kampuni ya Finland kwa jina HMD Global ambayo ilipata haki na idhini ya kuunda na kuuza simu za Nokia.
Kampuni hiyo ilijipatia umaarusu sana katika Maonesho ya Dunia ya Simu za Rununu mwaka 2017 ilipozindua simu za 3310 pamoja na simu nyingine za kisasa zenye nguzu zaidi.
Yamkini kampuni hiyo ililenga kurudia ufanisi wa mwaka jana katika maonesho ya mwaka huu wikendi mjini Barcelona.
Nokia 8 SiroccoNokia
Pamoja na kuundwa kwa chuma, Nokia 8 Sirocco pia haiwezi kuingia maji na haiwezi kusumbuliwa na vumbi
“Mwaka uliopita ulikuwa kuhusu kuzindua upya biashara ya simu za kisasa za Nokia,” alisema Ian Fogg kutoka shirika la ushauri la IHS Technology.
“HMD walianza kuuza simu hizo nchi za nje miezi saba ya mwisho mwaka 2017, na katika kipindi hicho walifanikiwa kuuza zaidi ya simu 8 milion
“Hii ina maana kwamba kwa idadi ya simu, wamewapita HTC, na Sony na pia Lenovo – kampuni ambazo zimekuwepo kipindi chote sokoni.”
HMD walisema katika kikao na wanahabari kwamba waliuza simu 70 milioni za aina mbalimbali mwaka 2017.

Simu ya chuma

Nokia 8 Sirocco inatumia mfumo kamili endeshi wa simu wa Android Oreo.
Hii ni tofauti na simu nyingine ambazo hubadilisha muonekano wa mfumo huo endeshi wa simu.
Nokia 8 Sirocco
Simu hiyo ya Nokia ina skrini iliyojipinda ambayo nje yake inashikiliwa na fremu ya chuma cha pua
Simu hiyo hata hivyo imerejesha tena uwezo wa Pro Camera ambao Nokia walikuwa wameuweka kwenye simu zao.
Hii inawawezesha wanaozitumia simu hizo kudhibiti kikamilifu wenyewe shughuli ya kupiga picha.
Uamuzi wa kutumia fremu ya chuma cha pua unafuata uamuzi sawa na wa Apple walipounda iPhone X, lakini bei yake ni ya chini.
Sirocco itagharimu euro 749 ($921; £659) itakapoanza kuuzwa Aprili.
“Historia imeonesha kwamba watu wengi huweka simu zao mifuko ya nyuma, na wanapoketi simu hizo huharibika,” anasema Ben Wood kutoka shirika la CCS Insight consultancy.
“Hivyo, hii ni mbinu nzuri ya kusaidia simu hizo ziwe za kipekee sokoni.”
Uamuzi wao wa kutumia kiendesha simu cha Qualcomm 835 badala ya 845 hata hivyo huenda ukawavunja moyo baadhi ya wateja.
New range of Nokia phonesNokia
Simu za sasa za Nokia zinazouzwa sokoni – ikiwa ni pamoja na Nokia 1, Nokia 6 na Nokia 7+

Simu ya ndizi

HMD pia wamezindua simu nyingine tatu za Android, ingawa zinaweza kuzidiwa sifa na 8110.
Ni simu ya kawaida tu, ambayo ina programu tumishi kadha (app) na inatumia mfumo endeshi wa Kai.
Miongoni mwa app hizo kuna Google Assistant, Google Maps na Facebook lakini hakuna app ya Twitter, Snapchat au WhatsApp.
Nokia 8110
Nokia wanapanga kufaidi kutokana kwa wanaokumbuka ya zamani kwa simu hii
Simu ya 8110 imejipinda kidogo – jambo lililosababisha simu awali kuitwa ‘simu ya ndizi’.
Ina kifuniko cha kibodi ambacho kinateleza na kufunika kibodi wakati mtu haitumii.
Lakini tofauti na simu iliyoonekana kwenye filamu ya The Matrix, kifuniko hicho hakitelezi kivyake, lazima kisongeshwe kwa mkono.
Simu hiyo inauzwa euro 79 ($97; £69). 
Ben Wood kutoka CCS Insight anasema: “Watu wanapenda vya zamani, na muhimu zaidi ni ya 4G. Hiyo ina maana kwamba inaweza kutumiwa kwenye mitandao mingi zaidi ya 3310, ambayo zamani ilikuwa ya 2G.”
KWA HISANI YA BBC Read More

Share.

About Author

Comments are closed.