Wednesday, August 21

Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco Yetu) limekanusha uzushi huu

0TAARIFA KWA UMMA 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linakanusha vikali taarifa inayo sambaa katika mitandao ya kijamii kuwa kutakuwa na tatizo katika mfumo wa manunuzi ya LUKU kuanzia tarehe 25 Machi 2018 hadi 05 Aprili 2018 , kwamba wateja wanunue umeme wa kutosha katika kipindi hicho. 

Taarifa hii si ya kweli, ni taarifa ya uzushi yenye nia ya kupotosha umma , kwani TANESCO haijatoa taarifa yoyote kuhusu hitilafu katika mifumo ya manunuzi ya LUKU. 

Ikumbukwe kwamba Taarifa kwa umma kutoka TANESCO hazitolewi na mtu binafsi bali Ofisi ya Uhusiano iliyo chini Idara ya Mkurugenzi Mtendaji ambayo ni msimamizi wa utoaji Taarifa za Shirika .

Tunaomba wateja wote wa TANESCO waipuuze taarifa hiyo kwani haina ukweli wowote. Wateja wote mnaombwa kuendelea kutumia huduma za umeme kama kawaida. 

TANESCO ‘‘Tunayaangaza Maisha yako’’ 


Kwa mawasiliano 

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii 

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Tanesco Yetu

IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO 
TANESCO MAKAO MAKUU 

MACHI 22, 2018Read More

Share.

About Author

Comments are closed.