Monday, August 19

Sergio Ramos aichuria Hispania, Ataja mataifa yenye nafasi ya kuchukua kombe la dunia

0


Beki kisiki wa timu ya taifa ya Hispania, Sergio Ramos ameiweka nje kando timu yake ya taifa kwenye mbio za kuwania kombe la dunia nchini Urusi mwaka huu.

Sergio Ramos
Ramos amesema kuwa anazipa nafasi kubwa timu za taifa za Ujerumani na Argentina kuchukua ubingwa wa Kombe la Dunia.
Nadhani Ujerumani na Agentina hii ya Messi zina nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa wa kombe la dunia mwaka huu,“amesema Sergio Ramos kwenye mahojiano yake na Waandishi wa Habari jana baada ya mazoezi mjini Madrid.
Leo Hispania itavaana na Argentina kwenye mchezo wa kirafiki unaotarajiwa kuwa na msisimko mkubwa usiku wa leo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.