Saturday, August 24

Ngorongoro Heroes yaipiga Msumbiji 2-1

0


Kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka ishirini, Ngorongoro Heroes, kimeibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Msumbiji jioni hii.

Ushindi huu umekuwa wa pili mfululizo, baada ya kuifunga pia Morocco katika mchezo uliochezwa Machi 18 2018 jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Ngorongoro yamefungwa na Abdul Suleimani katika dakika ya 35 na Saidi Mussa akifunga kwenye dakika ya 71, bao la kufutia machozi upande wa Msumbiji limefungwa na Leonel Victor katika dakika ya 13.

Matokeo haya yanaipa nafasi nzuri Ngorngoro kuelekea mchezo wake wa kuwania kufuzu kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana (AFCON U20) dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mechi itapigwa Machi 31 2018 kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Read More

Share.

About Author

Comments are closed.