Sunday, August 25

Mtalii afunguka baada ya Duma kuingia ndani ya gari Serengeti Tanzania (Video)

0


Mtalii Britton Hayes na mjomba wake kutoka Washington, Marekani wakiwa safarini katika mbuga ya Taifa ya Serengeti Tanzania kujionea wanyama, walijikuta katika wakati mgumu baada ya mnyama duma kuingia katika gari yao na kukaa zaidi ya dakika 10.

Mnyama huyo ambaye hakutarajiwa alikaa ndani ya gari hilo kwa dakika 10 katika eneo la Gol Kopjes la mbuga hiyo, kabla ya mwishowe kuondoka kwenda kuwinda swara.
Britton Hayes anasema wakati duma huyo anaingia alikuwa anamuangalia duma mmoja aliyekuwa ameruka sehemu ya mbele ya gari lao kumbe kuna mwingine aliruka na kuingia kupitia sehemu ya nyuma bila wao kumuona.
“Tulianza kugundua duma hao walikuwa wameanza kuvutiwa na gari letu; lakini hatukuwa na muda wa kuondoka au kutoroka kwa sababu hutaki kuwashtua wanyama hao, ukifanya hivyo ndivyo mambo huenda mrama,” Hayes aliambia jarida la Komo News.
“Nilikuwa nimejawa na wasiwasi sana. Lakini wakati wote nilikuwa nauhisi uhai wangu,” anasema.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.