Sunday, August 18

Mbwana Samatta apiga bao lake la 15 Stars ikiifundisha somo DR Congo uwanja wa Taifa

0


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta hii leo amefanikiwa kufunga bao lake la 15 wakati Taifa Stars ilipo ikabili DR Congo mchezo wa kirafiki ya kalenda ya FIFA.
Samatta amefunga bao hilo la 15 akiwa ameitumikia timu hiyo jumla ya michezo 40 na kuisaidi Stars kuchomoza na ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya Congo wakati lapili likifungwa na Shiza Ramadhani Kuchuya.
Licha ya kuwa na uwezo mkubwa kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo kimejaa mastaa wengi zaidi ukilinganisha na Stars wakiwa na wachezaji 4 wanao cheza nyumbani, 22 wakiwa wanacheza barani Ulaya na 14 kati ya wachezaji wote wa timu hiyo wamezaliwa Ulaya.
Viwango vya soka Dr Congo inashika nafasi ya 39 kwa ubora duniani na nafasi ya 3 kwa Afrika, Tanzania ikiwa ya 146 duniani na ya 44 kwa Afrika.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.