Sunday, August 18

Benki ya Stanbic yazindua mpango wa kukuza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi

0


Washiriki wa program inayoendeshwa na Benki ya Stanbic yenye lengo la kukuza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi wakiwa katika picha ya pamoja na mwendeshaji wa program hiyo, Patricia Murugambi (kati) wakati wa uzinduzi wa program hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Ken Cockerill akizungumza wakati wa uzinduzi wa program maalumu ya kukuza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi ndani ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana

21 Machi 2018, Dar es Salaam. Benki ya Stanbic Tanzania imezindua programu maalumu ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wake wa kike ili kushika nafasi za juu za uongozi ndani ya benki hiyo.
Akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango huo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Ken Cockerill alisema: “Kama mwajiri anaelenga kutoa fursa sawa kwa wafanyakazi wake, tumejitolea kuimarisha usawa katika shughuli zetu zote. Hii ni pamoja na kuhakikisha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kufikia nafasi za juu ndani ya benki. Mpango huu unalengo la kuendeleza viongozi wa kike ndani ya benki na, kwa kufanya hivyo, kuamsha ari na fursa ndani ya watu wetu.”
Aliongeza kuwa: “Suala hili tumelipa kipaumbele sio tu kwa sababu ni jambo sahihi kufanya, bali tafiti mbambali za kibiashara zinaonyesha kuwa uwepo wa uwiano wa kijinsia katika uongozi unasaidia kuleta manufaa makubwa ya kiutendaji.”
Mkuu wa kitengo cha rasimali watu wa benki hiyo, Bi. Eutropia Vegula alisema programu hiyo inayosimamiwa na chuo cha biashara cha Strathmore, itaendeshwa kwa muda wa miezi 6 na kushirikisha wanawake 25. Mada mbalimbali zitazungumziwa, zikiwemo kutafuta usawa wa kazi na maisha, ujasiri wa kuthubutu, na kufikiria kimkakati miongoni mwa mada nyingine nyingi.
“Mpango huu umelenga kuwajengea uwezo wanawake ili waweze kumudu vyema majukumu ya kiuongozi. Nataka kuchukua fursa hii kuwahamasisha wanufaika wa mpango huu kutumia mafunzo haya ili kuwainua wengine kupitia mienendo, mitazamo na utendaji wao,” alihimiza.
Mwisho/Read More

Share.

About Author

Comments are closed.