Tuesday, August 20

Wigan Athletic vs Man City inanikumbusha muujiza wa Roberto Martinez 2013

0


Ilikuwa mwaka 2013 kuelekea mchezo wa fainali ya FA kati ya Manchester City na Wigan, mchezo huu ulikuwa na habari nyingi sana kabla ya mechi lakini kubwa ilikuwa kibarua cha Roberto Mancini kuwa mashakani.

Pamoja na hilo lakini kila mtu aliamini Manchester City anakwenda kubeba FA kwani Wigan walionekana dhaifu sana na tayari walikuwa wamechungulia kaburi la kushuka daraja katika msimu huo.

Wachezaji wa City hawakuwa wanaelewa nini haswa kitamtokea kocha wao na labda waliwaza hilo, lakini upande wa pili Roberto Martinez alikuwa akiwaandaa wachezaji wake kisaikolojia kuelekea siku hii.

Wigan walifanikiwa kuwamudu Manchester City vilivyo na zikiwa zimebakia dakika sita kwa mchezo kukamilika Ben Watsons aliweka mpira kambani huku miezi sita iliyopita alikuwa amevunjika mguu.

Lakini Wigan hawajufurahia sana ushindi wao wa FA kwani siku tatu tu baadaye baada ya kubeba kombe walishuka daraja huku Manchester City nao masaa machache baada ya kipigo walimfukuza Mancini.

Leo wanakutana tena huku Wigan wakiwa na rekodi nzuri sana mbele ya City kwani mara mbili za mwisho kwa timu hizi kukutana katika FA, Wigan waliifunga City (fainali 2013 na robo fainali msimu uliofuata).

Mechi ya kwanza kabisa kwa vilabu hivi kukutana katika mashindano ilikuwa mwaka 1971 ambapo Manchester City waliibuka kidedea kwa ushindi wa bao moja kwa nunge bao la Colin Bell’s.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.