Monday, August 19

Tuchel aitosa Bayern Munich ili ajiunge na Arsenal, Wenger agoma kuondoka

0


Habari mpya zimeibuka kuhusiana na kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel ambaye Bayern Munich walikuwa wakimmezea mate wakimuona kama mrithi wa kocha wao mkuu wa sasa Jupp Heynckes.

Ripoti kutoka nchini Ujerumani zinadai ya kwamba Tuchel ameweka wazi kwamba kama baada ya kuifundisha Dortmund hana ndoto tena kubaki katika ligi ya Bundesliga jambo linaloashiria kuiva kwa safari yake kuelekea EPL.

Gazeti maarufu la michezo nchini Ujerumani la Bild limesema kwamba Arsenal ndio klabu ambayo kwa sasa inaonekana kwa asilimia kubwa kwamba wana uwezo wa kuwa na kocha huyo msimu ujao.

Tayari Tuchel yuko karibu na baadhi ya maofisa wa klabu ya Arsenal ambapo anatajwa kuwa ni moja ya kati ya watu waliosaidia upatikanaji wa Pierre Aubameyang katika klabu ya Arsenal kutokana na ukaribu wake na baadhi ya scout wa Arsenal.

Lakini wakati Tuchel akihusishwa na kujiunga na klabu ya Arsenal, kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesisitiza kwamba hataondoka katika klabu hiyo, Wenger amesema anakubaliana na changamoto zote lakini mpango wa kuondoka Gunners kwa sasa haupo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.