Saturday, August 24

Swansea na rekodi yao nzuri OT, kuwashangaza United hii leo?

0


Bado siku saba tu kwa Manchester United na Man City kukutana katika derby ya jiji la Manchester mchezo ambao utawakutanisha wakazi wa Dar Es Laam pale Escape One kuuangalia kwa pamoja.

Lakini kabla ya siku hiyo kufika, hii leo Manchester United wataikaribisha Swansea, wenyeji wa mchezo huu wanaonekana wagumu sana katika uwanja wa nyumbani wa Manchester United.

Katika michezo mitano iliyopita ya Swansea katika dimba la United wameshinda mara mbili na suluhu moja na hii inaonesha wastani mzuri wa matokeo kwa upande wao katika dimba la Old Traford.

Lakini tayari msimu huu United wameshawapiga Swansea mara mbili(uwanjani kwao) mechi moja ikiwa ni ya Epl (4-0) pamoja na kikombe cha ligi(2-0) hii ikimaanisha wamewafunga bila wao kuruhusu wavu wao kuguswa.

Lakini tangu Jose Mourinho ajiunge na ligi kuu nchini Uingereza Epl hajawahi kupoteza mchezo kwa Swansea huku akiwa amefanikiwa kuwafunga katika michezo saba na kutoka sare michezo miwili.

Tangu kocha Carlos Carvalhal aichukue Swansea wameonekana kuimarika zaidi kitimu ambapo katika michezo yao 8 iliyopita ya ugenini wamepoteza mchezo mmoja tu ila wameshinda mmoja na suluhu sita.

Paul Pogba anaweza kuwepo katika kikosi cha kwanza cha Manchester United huku akiwa na rekodi nzuri mbele ya Swansea kwani katika mechi zote alizocheza dhidi yao alifunga.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.