Saturday, August 17

Rekodi zilizowekwa hii leo wakati Manchester wakipeleka kilio London

0


Manchester City wameifikia rekodi ya Manchester United ya kuwa na makombe mengi ya ligi baada ya ushindi wao wa mabao 3 dhidi ya Arsenal na sasa City nao wanakuwa na makombe 5 ya ligi kama United.

Taji hili limeendeleza ukame kwa Arsene Wenger wa makombe lakini hili limekuwa kombe la kwanza kwa Pep Gurdiola tangu afike nchini Uingereza na huku likiwa la 22 tangu aanze ukocha.

Bao la leo la Kun Aguero lilikuwa bao lake la 199 kwa klabu lakini likiwa bao lake la 30 kwa msimu huu, hii ni mara ya 4 kwa Sergio Kun Aguero anafunga mabao 30 katika misimu aliyokuwa Manchester.

Kwa upande wa majirani wa Man City ambao ni United Romelu Lukaku amewajibu Chelsea baada kwa mara ya kwanza kuifunga timu iliyoko 8 bora na kunyamazisha kelele kwamba anazionea timu ndogo.

Lakini pia Lukaku alitoa assist ya bao la Jesse Lingard na hili lilikuwa bao la 10 kwa United kutoka kwa wachezaji wa akiba, idadi ambayo hakuna timu ambayo sub wake wamefunga mabao mengi kama hii.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.