Sunday, August 25

Paul Pogba hawezi kuwa na furaha Manchester United

0


Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps ameibuka na kusema kwamba kiungo wa klabu ya Manchester United Paul Pogba hawezi kuwa na furaha chini ya kocha Jose Mourinho.

Pogba kwa sasa yuko na Deschamps baada ya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Colombia na kocha wake anamuona nyota huyo hayuko sawa.

Deschamps anamsikitia Pogba kutokana na maisha yanavyomuendea katika klabu ya Manchester United katika siku za karibuni na kuwekwa kwake benchi katika mechi za usoni ikiwemo mechi kubwa dhidi ya Liverpool.

Kocha huyo wa Ufaransa amesisitiza kwamba kinachomtokea Pogba kwa sasa hakikubaliki kwani nyota huyo anajitahidi kuwapa Manchester United kila wakitakacho lakini bado hapewi nafasi.

Hali inayomtokea Paul kwa sasa ni hatari kwake hasa kuelekea michuano ya kombe la dunia kwani kama kiungo huyu ataendelea kukosa namba ndani ya United inaweza kumplekea kuanza kupoteza namba pia katika timu ya taifa Ufaransa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.