Friday, August 23

Michezo hii ya leo inaweza kutoa picha ya kombe la dunia

0


Michezo ya kirafiki ya mataifa inaendelea, jana tumeshuhudia time yetu ya taifa ikifa mabao manne kwa moja, lakini huko narani Ulaya nako kuna mechi kali wiki hii ambazo huwezi kuuacha kuzitizama.

Urusi vs Brazil, mchezo muhimu kwa wenyeji wa kombe la dunia kujipima dhidi ya taifa ambalo linapewa nafasi kubwa kubeba kombe la dunia. Huu ni mchezo muhimu pia kuwaona Brazil wanavyoweza kucheza bila Neymar ambaye ni majeraha.

Wakati watu wakiangalia ufundi katika mchezo huu pia ni muhimu kuangalia dimba ambalo litatumika kucheza fainali za kombe la dunia msimu huu dimba la Luzhniki Stadium, Douglas Costa na Roberto Firminho wanaweza kuwa wachezaji wa kuangaliwa hii leo.

Argentina vs Italy, huwezi kuacha kuangalia mchezo ambao unakutanisha miamba kama hii, pamoja na kwamba Italia hawapo kombe la dunia lakini bado ni taifa lenye heshima kubwa na kugopwa katika soka.

Achana na Lionel Messi, timu ya taifa ya Argentina imekuwa na tatizo kubwa katika ulinzi na hili linatazamwa kama janga la Waargentina na ni kati ya vitu Waargentina wanataka kuona vikitibiwa kabla kombe la dunia halijaanza.

Ujerumani vs Hispania, hii ni nusu fainali ya kombe la dunia 2010 ambapo Hispania walishinda, leo Hispania inakutana na Ujerumani timu ambayo ni ya kuogopwa sana kombe la dunia.

Wengi wanaamini kama sio Brazil baasi Ujerumani atabeba kombe la dunia, kipimo sahihi cha suala hili ni michezo ya aina hii lakini pia uwezo wa Hispania unaonekana kupwaya na mchezo huu unaweza kutoa picha halisi.

France vs Colombia, Paul Pogba anaweza kuwa sababu ya kuutazama mchezo huu, wanadai hana kiwango kizuri United kwa kuwa Mourinho hawezi kumtumia lakink wengi watataka kuona kama Didier Dechamps anaweza kumtumia?

Sio mchezo mrahisi kwani Colombia mara zote wamekuwa kati ya timu ngumu sana kutoka America Kusini, hii inaifanya mechi ya leo kuwa mchezo mgumu na mzuri sana kuutizama.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.