Saturday, August 24

Mchezaji apiga soka dakika 90 huku jana yake akitoka kufiwa na mwanae

0


Hii imetokea nchini Iraq siku ya jana na ni kati ya habari ambazo hii leo imewagusa wengi sana na wengi wameku wakiisoma kwa masikitiko makubwa kutokana na habari inayomhusu mchezaji Alaa Ahmed.

Ahmed ni golikipa wa klabu ya Naft Maysan inayoshiriki ligi kuu nchini Iraq na siku ya jana alikuwepo uwanjani wakati Maysan wakicheza mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Al Shorta mchezo ulioisha kwa suluhu.

Lakini wakati mchezo unaendelea hakuna aliyejua nini kipo kwenye kichwa cha Alaa Ahmed na laiti kama wenzake na kocha wa timu yao angejua baasi wasingemchezesha mlinda lango huyo siku hiyo .

Ahmed siku moja kabla ya mchezo alifiwa na mtoto wake na hakumuambia mtu yeyote kuhusu kifo hicho hadi mchezo ulipoisha ndipo alianza kulia sana na wachezaji wenzake walimuuliza ndipo akawaambi kilichomtokea.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.