Sunday, August 25

Matokeo ya mechi kubwa za kirafiki hii leo, Hispania watuma salamu

0


Baada ya michezo 20+ bila kupoteza mchezo hata mmoja, hatimaye hii leo timu ya taifa ya Ujerumani imeonja kipigo baada ya kufungwa bao moja kwa nunge kutoka kwa Brazil ,bao likiwekwa kimiani na Gabriel Jesus(37).

Timu ya taifa ya Uingereza imeshindwa kuendeleza wimbi la ushindi baada ya hii leo kukubali suluhu ya bao moja kwa moja dhidi ya Italia, Uingereza walipata bao kupitia Jamie Vardy kabla ya Lorenzo Insigne kusawazisha kwa penati.

Aibu iliwakuta Argentina baada ya kukubali kipigo cha mbwa mwizi kutika kwa Hispania cha mabao 6 kwa 1, huku Isco akiweka kambani hat trick, Diego Costa, Iago Aspas na Thiago Alcantara wakiichakaza Argentina iliyokuwa bila Lionel Messi.

Dozi waliyotoa leo Hispania inaweza kuwa kama salamu kwa timu nyingine za taifa kukaa chonjo haswa kwa wakati huu ambao watu walishaanza taratibu kuitoa  Hispania katika timu tishio duniani.

Romelu Lukaku alifunga mabao mawili wakati Ubelgiji ikiifunga Saudi Arabia mabao 4 kwa nunge huku mabao mengine yakifungwa na Kelvin De Bruyne pamoja na mshambuliaji wa BvB Michy Batshuayi.

Wawakilishi wa Afrika Nigeria walikubali kipigo cha bao mbili kwa nunge toka kwa Serbia na mabao yote yakifungwa na Aleksandar Mitrovic, Misri walifungwa bao moja na Ugiriki huku Senegal wakienda sare na Bosnia. Read More

Share.

About Author

Comments are closed.