Tuesday, August 20

Manchester United wana mkosi katika ardhi ya Hispania, Mourinho anaweza kuufuta?

0


Hii leo usiku Manchester United watakuwa nchini Hispania ambako wamekwenda kuwakabili wenyeji wao Sevilla katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya klabu bingwa Ulaya, mchezo ambao ni muhimu sana kwa United.

Lakini United hawana furaha kutokana na rekodi yao ilivyo mbovu katika taifa la Hispania, katika miaka 51 iliyopita United wamekwenda nchini Hispania mara 23 lakini wakafanikiwa kushinda mara 3 tu.

Lakini hii leo kutokana na ubora wa kikosi chao, United wanapewa nafasi kubwa kuibuka kidedea mbele ya Sevilla, na pia United wana kumbukumbu ya mchezo wao wa mwisho nchini Hispania walipoifunga Celta Vigo katika mchezo wa nusu fainali ya Europa.

Ukiacha ushindi wa Manchester United dhidi ya Celta Vigo lakini pia mwaka 2002 mwezi April mabao ya David Beckham na Ruud Van Nistelrooy yaliwafanya Manchester United kuibuka kidedea katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Deprtivo La Coruna.

Lakini yote tisa ila kumi ni kumbukumbu kubwa ya Manchester United katika ardhi ya Hispania ambapo ilikuwa mwaka 1999 wakati United wakiifunga Bayern Munich katika fainali ya michuano hii.

Ila michezo hiyo ndiyo michezo pekee United walipata ushindi nchini Hispania na wana kumbukumbu ya vipigo ikiwemo kipigo kikubwa zaidi cha mabao 4 kwa nunge walichopewa na Barcelona 1994/1995.

Msimu wa 1983/1984 Barcelona wakiongozwa na Diego Maradona waliichapa tena United bao 2 kwa nunge nchini Hispania japokuwa baadaye United walibadili matokeo hayo na kuwachapa Barcelona bao 3 katika dimba la Old Traford.

Real Madrid nao wamekuwa wakiwaonea sana Manchester United wakija Hispania, waliwapiga 3-1 katika nusu fainali ya Europena Cup msimu wa 1956/1957 na msimu wa mwaka 2002/2003 Real Madrid wakawapa tena United kipigo kama hicho katika robo fainali ya Champions League.

Timu nyingine zinazowapa United historia chungu katika ardhi ya Hispania ni pamoja na Villareal, Real Sociedad pamoja na Athletico Madrid lakini kwa Villareal hii leo itakuwa mara yao ya kwanza kukutana na United katika mashindano.

Villareal wanaweza kuendeleza mkosi wa Manchester United nchini Hispania au kocha Jose Mourinho anaweza kubadilisha mambo na kuendeleza kile walichofanya mara ya mwisho walipofika Hispania.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.