Friday, August 23

Kuanzia kwa Mao, Manyika hadi Kluivert,hawa ni baba nwa mwana waliong’ara katika soka

0


“Maji hufuata mkondo” waswahili ndio wamesema hivyo, hili linadhihirika pia katika soka kupitia baadhi ya nyota wa soka ambao wanacheza soka kufuata nyayo za wazazi wao, hawa ni baadhi yao.

Mao Mkami na Himid Mao, nani asiyemjua “Ball Dancer” nyota wa zamani wa Mtibwa na Pamba, Mao Mkami ni baba mzazi wa nyota wa sasa wa Azam Fc na timu ya taifa ya Tanzania Himid Mao.

Salum Abubakar na Abubakar Salum,  kiungo wa Azam Salum Abubakar “Sure Boy” mara nyingi amekuwa akidaiwa kuwa na mapenzi na klabu ya Yanga, hii ni kutokana na baba yake mzazi mzee Abubakar Salum kuichezea Yanga enzi za uchezaji wake.

Manyika Jr na Peter Manyika, mtoto wa nyoka ni nyoka na hili linadhihirika kwa mlinda lango huyu wa Singida United , baba yake mzazi ambaye ni Peter Manyika alikuwa akiidakia Yanga hapo zamani.

Justin na Patrick Kluivert, Justin ni nyota wa soka ambaye siku za usoni amekuwa akizungumziwa sana, winga huyu wa Ajax anaonekana kufuata nyayo za baba yake Patrick Kluivert ambaye naye enzi zake aliweka kambani mabao 40 katika michezo 79.

Mazinho, Thiago na Rafinha. Mazinho alikuwa alikuwepo katika kikosi cha timu ya taifa Brazil mwaka 1994 na sasa anafuraha kuwaangalia watoto wake wawili Thiago ambaye anaichezea Bayern Munich na Hispania huku Rafinha akiichezea Inter na Brazil.

Peter na Kasper Scheimiechel, hawa ndio baba na mwana ambao wana uhusiano kabisa wa kidamu na kubeba EPL, Peter alibeba akiwa mlinda lango wa United huku Kasper akifanya hivyo akiwa mlinda lango wa Leicester.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.