Thursday, August 22

Je wajua? Kuna makocha 8 La Liga ambao wako kama Zidane?

0


Zinedine Zidane “Zizzou” ni kocha mwenye mafanikio kwa sasa La Liga lakini pia Zizzou amewahi kuitumikia Real Madrid kama mchezaji, lakini la Liga sio Zidane pekee aliyewahi kuwa mchezaji na baadae kocha.

Diego Simeone, msimu wa mwaka 1995/1996 alifunga moja ya bao wakati Athletico Madrid wakitwaa kombe la ligi, baadae alitundika daluga lakini alirejea tena Athletico kama kocha na kuipandisha timu kuwa kati ya timu za kuogopwa Ulaya.

Ernesto Valverde ,msimu wa mwaka 1988/1990 Valverde alikuwa akiichezea Barcelona akifanikiwa kufunga mabao 8 katika mechi 22 na safari hii yuko kama kocha huku msimu huu wakitarajiwa kufanya makubwa.
Kuko Ziganda, José Ángel “Kuko” Ziganda alikuwa nyota Athletic Bilbao mwaka 1991/1998 akifunga mabao 77 katika kipindi hicho lakini sasa mambo yanamuendea kombo kama kocha ambapo hadi sasa Bilbao wako nafasi ya 13.

Abelardo, inaonekana huyu hataki kukumbuka kile kilichowatokea Alaves mwaka 2002/2003 walishuka daraja kwani safari hii wako katika nafasi nzuri ya kutoshuka daraja.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.