Thursday, August 22

Huyu ndio “pass master” Epl hadi hivi sasa

0


Ligi kuu nchini Uingereza iko katika mapumziko kupisha michezo ya kimataifa ya kirafiki, lakini takwimu mbali mbali za ligi hiyo bado zinaendelea kukusanywa na hii ni orodha ya wanaopiga pasi zaidi na kukamilika katika eneo la wapinzani Epl.

05.Mesut Ozil, huyo ni kati ya nyota ambao tangu ajiunge la ligi kuu nchini Uingereza amekuwa na muendelezo mzuri hasa katika assist, hadi sasa Ozil amepiga pasi 1181 katika eneo la wapinzani na zikafika kwa walengwa.

04.Fernandinho, Pep Gurdiola anaonekana kufanya jambo kubwa sana na muhimu kwa kumuamini sana Mbrazil huyu msimu huu, na hajamuangusha kwani achilia mbali ukabaji wake ila hadi sasa Fernandinho amekamilisha pasi 1212.

03.David Silva, huwezi ukataja wapiga pasi Epl kwa sasa ukamuacha Silva, ndio engine ya City na nafasi nyingi huwa zinaanzia kwake. Hadi sasa raia huyu wa Hispania ameshapiga jumla ya pasi 1272 katika eneo la wapinzani na zikafika.

02.Kelvin De Bruyne, huwezi kumtaja Silva halafu ukamuacha De Bruyne, hawa wawili kwa pamoja wanaendesha timu na ndio wanaifanya City icheze, hadi sasa De Bruyne amepiga pasi 1337 katika eneo la wapinzani.


01.Granit Xhaka, usimchukulie poa hata kidogo Xhaka, pamoja na utemi wake wote lakini Xhaka ndiye mchezaji kinara wa kupiga pasi katika eneo la wapinzani, amepiga pasi 1351, huku jumla akikamilisha pasi 2134.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.