Saturday, August 17

Hii ndio sababu kubwa ambayo United wanashangilia sana suluhu vs Sevilla

0


“David De Gea ni aina ya magolikipa ambao wanawajaza washambuliaji uwoga, ukimkaribia unaweza kujiuliza hivi kweli nitaweza kumfunga?” Sio maneno yangu ni maneno ya Frank Lampard baada ya mechi ya United.

Wakati wa mapumziko hata mtangazaji wa mechi hiyo alishangaa ni kwanini matokeo ni bila bila kutokana na nafasi ambazo Sevilla walikosa na kikwazo kikubwa ilikuwa mikono ya De Gea na sasa mshindi atakwenda kujulikana Old Traford.

Lakini habari ya kuwafurahisha United ni kwamba katika mechi 3 za mwisho ambazo hatua ya mtoano mechi ya kwanza walitoka suluhu ya bila bila walifanikiwa kufudhu.

Na sio kufudhu tu bali United walifanikiwa kwenda hadi fainali ,kama unakumbukua matokeo kama haya na Barcelona 2007/2008, wakaja tena na Inter 2008/2009 na kisha Marseille mwaka 2010/2011.

Michezo yote hiyo mitatu mechi ya kwanza United walipata suluhu ya bila bila wakaja wakashinda mechi ya pili na kisha wakafanikiwa kwenda hadi fainali na pengine labda hili linawafanya United kufurahia wakiamini katika rekodi.

Katika mchezo mwingine uliopigwa usiku wa leo bao la Fred liliwapa Shakhtar waliokuwa nyumbani ushindi wa bao 2 kwa 1 dhidi ya wageni As Roma.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.