Thursday, August 22

Haya unapaswa kuyajua kabla ya mtanange kati ya Huddersfield vs Manchester United

0


Ni wiki ambayo Manchester United walikuwa wakiandamwa na habari nyingi huku kubwa ni kuhusu Paul Pogba kutokuwa na raha, jambo ambalo kocha wa Manchester United Jose Mourinho amelikanusha.

Lakini hii leo United watakuwa ugenini katika michuano ya FA kuwakabili Huddersfield ambapo wenyeji wa mchezo huo wameshinda mchezo mmoja tu kati ya mechi zao 13 za mwisho walizokutana na United.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa timu hizi mbili kukutana katika michuano ya FA kwani United wameshacheza na Hudders mara tatu na kati ya hizo United wakashinda mara mbili huku kipigo kikubwa walikitoa 1963 wakiwafunga bao 5.

Mshambuliaji mpya wa Manchester United Alexis Sanchez ameshiriki katika mabao 15 ya FA msimu huu katika mechi 15 alizocheza huku akifanikiwa kutoa assist saba pamoja na kufunga mabao nane.

Huddersfield hawajawahi kufudhu kwenda robo fainali tangu mara ya mwisho wafanye hivyo mwaka 1972 na wamepoteza michezo mitano ya mwisho ya hatua kama hii ikiwemo mchezo wao dhidi ya Man City msimu uliopita.

Rekodi zinaonesha kwamba timu mbili za mwisho ambazo ziliwatoa United katika hatua ya 16 bora zilibeba ubingwa wa michuano hiyo na timu zenyewe ni Liverpool mwaka 2006 na Arsenal mwaka 2003.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.