Friday, August 23

Hawa ndio nyota 8 wanaokaribia kuondolewa United

0


Inasemekana kwamba kocha wa Manchester United Jose Mourinho ana mpango wa kupunguza nyota 8 katika klabu hiyo, mpango ambao amepanga kuufanya katika dirisha lijalo la usajili.

Kwa sasa kumekuwa na maneno mengi kuhusu Luke Shaw ambaye amekuwa akishambuliwa mara kwa mara na Jose Mourinho na hii inamfanya kuwa njiani kuelekea nje ya Old Traford.

Lakini kwa upande mwingine Mourinho anatajwa kutofurahia kiwango cha Chriss Smalling naye anaweza kuuzwa dirisha lijalo la usajili pamoja na walinzi wengine Dalley Blind na Matheo Darmian.

Anthony Martial naye yuko mbioni kupitiwa na panga hilo pamoja na Wahispania wawili Juan Mata na Ander Herrera huku hali ya Paul Pogba nayo klabuni hapo ikiwa bado haieleweki nini kitatokea mbeleni.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.