Wednesday, August 21

Cristiano Ronaldo amekwisha?!aaaah wapi!

0


Amekwishaa, amekwisha! Hayo sio maneno yangu bali ni maneno ya watu wa soka, wanadai toka msimu huu umeanza Cr7 sii lolote na kiwango chake kinaelekea ukingoni kutokana na ukame wa mabao.

Lakink habari imebadilika na imebadilika zaidi usiku wa jana wakati Mreno akiweka kambani mabao manne katika mchezo wao dhidi ya Girona na kuanza kufuta minong’ono ya kuisha kwake.

Hii ilikuwa hattrick ya 50 kwa Cristiano Ronaldo tangu aanze soka na tishia zaidi ni kwamba mshambuliaji huyu amefunga jumla ya mabao 17 katika michezo 8 iliyopita aliyoichezea Real Madrid.

Kama unakumbuka mwezi November Cr7 aliahidi kushinda Pichichi (mfungaji bora La Liga) wakati huo ana bao 1 huku Messi ana mabao 11 na watu walimcheka Cr7, lakini sasa mambo yanaonekana kubadilika.

Mabao manne aliyoyafunga hapo jana yanampa Ronaldo jumla ya mabao 25 katika michuano ya La Liga ikiwa ni mabao 3 nyuma ya Lionel Messi na likiwa ni bao 1 juu ha Luis Suarez na sasa Madrid wamefikisha alama 60 katika michezo 29.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.