Tuesday, August 20

Almanusra Serena Williams apoteze maisha kutokana na ujauzito

0


Mwezi September mwaka jana aliyewahi kuwa mcheza tennis namba moja dunia Sereba William alibahatika kupata mtoto wa kike ambaye alimpa jina la Alexis Olympia Ohanian Junior.

Serena ambaye amewahi kushinda Grand Slam 23 ameelezea kitu ambacho watu wengi hajawahi kujua kuhusu ujauzito wake baada ya kusema kelezea jinsi alivyonusurika kufa wakati akimzaa Olympia.

Serena anaeleza kwamba moyo wake mapigo ya moyo yalishuka ghafla wakati akiwa katika hatua za mwisho kujifungua na hali hii ilipelekea kufanyiwa upasuaji ambao anashukuru mungu ulienda salama.

Historia ya uzazi ya Serena inamhatarisha wakati akiwa anajifungua na anaeleza kwamba hata ujauzito arteries ziligoma kufanya kazi na hii ikamfanya awe anapata tabu katika upumuaji hali iliyopelekea madaktari kumpelekea chumba cha upasuaji.

Serena anasema kwamba kutokana na rekodi alizonazo kuhusu afya yake ya uzazi anaishi kwa mashaka makubwa haswa akipata mimba kwani huwa anahofia kupoteza maisha katika nyakati kama hizo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.