Monday, August 19

MAMBO YA KUFANYA KULINDA AFYA YAKO DHIDI YA ATHARI ZA MAZINGIRA YA KAZI

0


Ajira ni sehemu muhimu sana katka maisha ya kila mwanadamu. Iwe ya kuajiriwa au kujiajiri umuhimu wake katika ustawi wa mtu mmoja mmoja, taasisi, jamii, nchi na dunia kwa ujumla ni mkubwa sana. Pamoja na umuhimu wake unaweza pia kuwa chanzo cha majanga mengi hasa ya kiafya.

Mazingira ya kazi yanatafsiri pana sana. Hayahusishi vitu vinavyoonekana au kutuzunguka tunapo kuwa kazini pekee laikin pia yanahusisha mahusiano yetu na watu wengine maeneo ya kazi au tunaohusiano nao kutokana na kazi au ajira zetu. Kwa kuona namna dhana ya mazingira ya kazi ilivo pana unaweza kupata picha ya kwa namna gani yanaweza kuhatarisha maisha yetu tusipokuwa makini maeneo ya kazi. Vipo vitu kadhaa vinavyoweza kuwa sababisha au kupelekea afya zetu kuathirika kwa namna moja ama nyingine. Mambo yafuatayo yanweza kukusaidia kuepuka au kupunguza madhara unayoweza yapata yatokanayo na mazingira ya kazi;

EPUKA KUFANYA MAJUKUMU KUPITA KIASI

Mwili wa binadamu unahitaji kupewa matunzo na moja ya njia ya kuhakikisha kuwa haudhuriki kilahisi na athari za kiafya ni kuupa muda mzuri wa kupumzika. Shughuli tunazozifanya wakati mwingine zinatunyima muda wa kupumzisha miili na akili zetu vya kutosha na hivyo kutufanya kuathirika hata kisaikoojia. Ni vyema kuhakikisha kuwa majukumu tunayopewa au kuyafanya hayazidi uwezo wetu. Uhuhusiano wa muajiri na mwajiriwa wakati mwingine unaweza kuwa sababu yaw engine kushindwa kuwa wa wazi juu ya kiwango cha majukumu wanachopewa. Jifunze kuzungumza vyema na bosi wako kwani siku atakaposhindwa kufanya kazi kwa sababu za kiafya mwajiri wako anaweza asiwe msaada na pengine anaweza kutafuta mtu mwingine.

JENGA MAHUSIANO MAZURI NA WENGINE

Mahusiano kati ya mtu na mtu katika mazingira ya kazi yana athari nyingi za kiafya hasa kisaikolojia zinazoweza kupekeleka athari nyingine. Unapokuwa hauna amani na furaha kazini kwa sababu ya kero za watu wanaokuzunguka usidhani kuwa ni jambo dogo. Kwa sababu tofauti tofati wapo watu makazini hawaongeleshwi hata na wafanyakazi wenzao wa karibu na hivyo kujikuta wakinuniwa tangu siku inapo anza mpaka inapoisha. Wengine ukali wa mabosi wao umekuwa pia kero ya kufanya mazingira ya kazi yasiwe rafiki kabisa. Hili linaweza kukuletea msongo wa mawazo, sonona na kufanya afya yako kuathirika.

Wakati mwingine mahusiano yanaweza yasiaribiwe na wewe lakini wanaokuzunguka. Jifunze kuondoa au kurekebisha tofauti za kimahusiano pale tu zinapojitokeza. Usiache na kudharua vitu vidogogo vinavyoweza kuwa vinakunyima amani na furaha kazini.

KULA MLO KAMILI NA KWA WAKATI

Ni dhahiri kuwa aina vyakula na muda wa kula mara nyingi unaathiriwa sana na mazingira ya kazi. Muda unao kula ukiwa nyumbani hutofautiana na ule unaokula ukiwa kazini n ahata aina ya vyakula pia uwa siyo vile tunavyovipata tukiwa majumbani kutakona na machaguo machache yaliyopo maeneo ya kazi.

Wakati mwingine kazi na majukumu yanakuwa mengi mpaka muda wa kawaida wa kula unapita. Wakati mwingine vyakula vinavyopatikana kwa haraka ni vile vyenye mafuta kupita kiasi vinavyoweza kuwa chanzo cha unene uliopitiliza au shinikizo la damu.

Ni vyema kujitahidi kupata mlo kamili na ule ambao hauta hatalisha afya yako. Kuwepo kazini si sababu ya lazima ya wewe kula chips kila siku. Hakikisha pia una kula kwa wakati uanofaa na siyo kukaa na njaa muda mrefu kwa sababu tu umebanwa na majukumu. Afya yako inatakiwa ipewe kipaumbele.

JIKINGE NA ATHARI ZA TEKNOLOJIA

Teknolojia imerahisisha sana maisha katika nyanja mbali mbali ikiwemo shughuli zetu za kila siku. Unatoka nyumbani kwako asubuhi na mapema ukiwa kwenye gari, ukifika ofisini haupandi ngazi unatumia lift, ukikafika ofisini ukitaka kujongea kutoka sehemu moja ya ofisi na kwenda nyingine hautembei bali unajivuta na kiti chako. Muda wa kazi ukifikika unashuka kwa lifti na unapanda gari kurudi nyumbani. Mazingira kama haya ni hatari sana kwa afya ya mtu yoyote yule. Yanatenegeneza uvivu kupita kiasi unaweza kuwa chanzo cha magonjwa mengine mengi. Mwili unahitaji kupewa mazoezi walau ya kutembea kwa dakika kadhaa ili kuimarisha afya lakini wakati mwingine shughuli zetu zinatunyima fursa hii na kujisahau hata kutenga muda wa mazoezi.

Tenga muda binafsi wa kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara. Wakati mwingine kwa umbali usiomrefu si lazima utumie gari; kutembea kunaweza imarisha afya yako. Wakati mwingine wawezatumia ngazi badala ya lift unayoitumia kila siku kupanda majengo marefu.

FANYA KAZI KWA TAHADHARI

Baadhi ya kazi kwa asili ni hatarishi. Mfano mzuri ni zile zinazofanywa viwandani, kwenye karakana na maeneo mengine. Kazi hizi zinamuweka mfanyakazi kwenye hatari kubwa ya kupoteza baadhi ya viungo, kupata majeraha, magonjwa na hata kifo. Sheria na mamlaka zinayohusika na kusimamia usalama mahala pa kazi zinamtaka mwajiri kuchukua tahadhari dhidi ya majenga yanayoweza kutokana na shughuli mbali mbali maeneo ya kazi. Hii inajumuisha wafanyakazi kuwa na mavazi maalumu ya kuwakinga na majanga hayo. Pamoja na matakwa ya kisheria wapo baadhi ya waajiri hupuuza huku baadhi ya wafanyakazi wakiona hakuna umuhimu wa kuchukua tahadhari hizi.

Hata katika ofisi nyingine za kawaida uwepo wa vifaa vya kuzimia moto, milango ya dharura na tahadhari nyingine nyingi zinahitaji kuchukuliwa ili kulinda afya za wafanyakazi na wateja wanaohudumiwa. Ni vyema wafanyakazi kuchukua tahadhari ili kuepuka madhara yanayoweza jitokeza. Hii iendane na wafanyakazi kujua na kudai haki zao za msingi kwa waajiri katika kulinda afya zao dhidi ya majanga yanayoweza jitokeza.

Share.

About Author

Leave A Reply