Thursday, August 22

TAIFA STARS YASUKWA UPYA, MANDAWA NDANI NA ULIMWENGU NJE, MABADILIKO MENGINE KADHAA YAKO HIVI

0 

Mshambuliaji Mtanzania, Rashid Mandawa anayeichezea klabu ya BDF XI ya Botswana,ameongezwa kwenye orodha ya wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Stars inajiandaa kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Algeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Taifa Stars itaanza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Algeria Machi 22 2018, kabla ya kuikaribisha nyumbani timu ya taifa ya Kongo, Machi 27 2018.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, awali aliita kikosi chenye jumla ya wachezaji 23 lakini baadhi wamepunguzwa kutokana na sababu mbalimbali.

Wachezaji walioitwa hapo mwanzo na sasa wameondolewa ni: Thomas Ulimwengu, Said Ndemla, Farid Mussa, Hamis Abdallah na John Bocco.

Walioongezwa na kufanya idadi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho kuwa 21 ni: Himid Mao, Rashid Mandawa pamoja na  Shaaban Idd.

Kikosi hicho kitaondoka hapa nchini kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kirafiki utakaopigwa Mach 22 2018.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.