Thursday, August 22

Singida United yajishauri kumpa mkataba Mudathir

0


Klabu ya soka ya Singida United bado haijaweka wazi endapo itamsajili kwa mkataba wa kudumu kiungo Mudathir Yahya, ambaye ameachwa na klabu yake ya Azam FC baada ya mkataba wake kumalizika.

Mudathir ambaye anaichezea Singida United kwa mkopo wa msimu mmoja kutokea Azam, kwasasa ni mchezaji huru baada ya Azam kuweka wazi kuwa hawataendelea naye hivyo kama kuna timu inamtaka inaweza kumpata akiwa huru.

Kwa upande wa Singida United bado hawajaweka wazi kama watafanya taratibu za kumsajili kwa mkataba wa kudumu kiungo huyo ambaye kwasasa amerejea timu ya taifa ya Taifa Stars baada ya kukosekana kwa muda.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema bado wanalishughulikia suala hilo na watalitolea taarifa kwa muda muafaka lakini kwasasa bado wanajua Mudathir ni mchezaji wao kwa mkataba wa mkopo.

”Ni kweli amemalizana na klabu yake ya Azam FC ambayo sisi tulimsajili kwa mkopo kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini kwasasa suala lake tunalishughulikia baada ya timu yake kuweka wazi kuwa haitaendelea naye na amemaliza mkataba kwahiyo ni mchezaji huru”, amesema.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.