Monday, August 19

SANCHEZ AKIRI KUKUTANA NA WAKATI MGUMU MANCHESTER, MAMBO YAKO HIVI

0


Mshambuliaji wa Manchester United, Alexis Sanchez, amesema alitarajia mambo kwenda sawa baada ya kujiunga na Manchester United January 2018.

Mchezaji huyo ameeleza hayo baada ya kuona mambo yanaenda tofauti na alivyotarajia mpaka sasa tangu aondoke Arsenal na kutua Old Trafford.

Sanchez mpaka sasa amepata nafasi moja tu ya kucheka na nyavu katika michezo 10 aliyoichezea Manchester United tangu ajiunge.

Aidha, Mshambuliaji huyu amekiri kuwa anahitaji kupambana zaidi ili kuweza kuzoea maisha mapya ndani ya United ambayo bado ni klabu ngeni kwake hivi sasa.

Sanchez alijiunga na United mapema January mwaka huu akitokea Arsenal, klabu ambayo alitumikiabaada ya kwa jumla ya misimu minne.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.