Sunday, August 25

England Wasusia Kombe Dunia

0


Hivi majuzi nilimwambia Rafiki yangu kuwa siamini kama Marekani walishindwa kufuzu kombe Dunia Urusi hasa ukitazamia washindani wake. Kuna siri kubwa ambayo hatujui. Yaan leo hii Marekani washindwe kwenda kombe la Dunia? Mhh hapana. Kidogo kwa Waitaliano unaweza ukaona logiki.

Marekan na Urusi ni watu waliokuwa kwenye mvutano mkubwa wa kisiasa. Utawaaminisha vipi wamarekani kwenda urusi? Warusi watawaamini vipi wamarekani ndani ya taifa lao?

Kati ya mambo ambayo FIFA wameshindwa kuyavumbua ni kuruhusu taifa lenye mvutano wa kisiasa kuandaa kombe la dunia.

Imezuka sintofahamu nyingine kwa waingereza hasa baada ya Vladmir Putin kurudi madarakani huku akitoa kauli za uchochezi dhidi ya njama za mauaji ya Jasusi mmoja wa KGB na mtoto wake wa kike jijini London. Putin amedai hahusiki na mauaji hayo. Kwa mantiki hiyo tuhuma zote zitaenda kwa Waingereza.

Madai haya yamemchefua sana waziri mkuu wa UINGEREZA Bi Theresa May. Familia ya kifalme Uingereza imekanusha vikali mauaji yale na inaamini fika kuwa Urusi wamehusika kwa kiasi kikubwa. Mpelelezi huyo bwana Sergei Skripal na mtoto wake kike Yulia walinusurika kuuwawa kitendo kikichofanya Taifa la Urusi kulaani kitendo kile.
Bi Theresa May amesema amevunja makubaliano ya aina yoyote na Urusi na wametupilia mbali ombi la waziri wa masuala ya kigeni wa Urusi bwana Lavrov kuingia England.

Hii manake nini? Athari kubwa kisoka zinakuja hapo.

Kama unavyojua Marekani na Uingereza ni mtu na shemeji yake kwa namna walivyokaribu. Sidhani kama hali ya amani itakuwa ya kutosha.

Kuna athari kubwa kwa timu ya taifa ya England kule Urusi. Kwanza hawatakuwa na uhuru huko ugenini kisaikolojia, pili Hata Mtoto wa mfalme Prince Willium ambaye ni raisi wa Shirikisho la Soka England FA, amesema hatoshiriki kombe la Dunia huko Russia kama alivyoahidi hapo awali. Hakuna mwana familia ya kifalme atakayekwenda. Je mashabiki wa kirusi watawachukulia vipi mashabiki wa malkia? Andrew Neil amesema haoni namna Russia itajitoa kwenye njama za mauaji ya Raia wake na hii italeta picha mbaya kwenye kombe la dunia.

Waziri mkuu wa England amesema kwanza warusi walileta hali ya tafrani katika mji Salisbury. Warusi waliingia kwa fujo katika mji huo kuchunguza tukio lile. Kwanza hawakupata vibali kutoka kwa serikali ya England kufanya uchunguzi huo. Ajenti huyo wa kirusi mwenye miaka 60 alikutwa yupo hoi baada ya kuwekewa sumu.

May alisema hahitaji ubalozi wake nchini Moscow wala hamtaki balozi wa Urusi nchini humo. Mwanamama huyo ameongeza kuwa yupo tayari kushikilia mali au chombo chochote cha kirusi ambacho kitaonekana ndani ya nchi hiyo kuathiri amani. yeye mwenyewe hata hilo kombe hana muda nalo.
Urusi nayo imejibu mapigo kuwa wamelaani majaribio ya Uingereza. Na wamelaani tuhuma za Bi May kuwa ni za uzushi Kwanza putin amesema hajali chochote ila anachojua hahusiki na mauaji hayo labda waingereza wajibu kipi kilimtokea raia wake.

Kombe letu la Dunia litakuwa na picha ya aina hii. Hii ni vita ya kisiasa lakini huenda ladha ya soka ikapotea. Na si unajua waingereza walivyo na mdomo unategemea nini?

Huenda hawa jamaa wakajitoa kombe la dunia aisee maana hawashindwi.
.
Imeandaliwa na Priva ABIUD 076337002

UPi mtazamo wako? Acha Comment yako hapo chini.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.