Wednesday, August 21

WAKAZI WA DODOMA KUFAIDI UHONDO WA TAMASHA LA PASAKA APRILI 8, 2018

0


Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya kuongeza mkoa wa DODOMA katika Tamasha la Pasaka 2018. Pembeni kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo, Jimmy Charles na Meneja wa Break Point ambao ni moja yawadhamini.

Wakazi wa Dodoma wanatarajia kufaidi uhondo wa Tamasha la Pasaka 2018 ifikapo Aprili 8, 2018 ndani ya Uwanja wa Jamhuri.

Akitangaza neema hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amesema kuwa haoni namna ya kuwanyima wakazi wa mji mkuu wa Tanzania, Dodoma uhondo wa Tamasha la Pasaka na baada ya kumaliza mazungumzo hatimaye ameamua kutangaza rasmi.

Msama amesema kuwa wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake hawana budi kulisubiria Taamasha hilo ambalo hufanyika mara moja tu kwa Mwaka.

“Wakazi wa Dodoma napenda kuwakaribisha kwenye Tamasha la Pasaka 2018, hauna haja ya kulikosa maana lenyewe hufanyika mara moja tu kwa mwaka na nyie mmeopata upendeleo wa Ajabu, Tutaanza na Kanda ya Ziwa ndani ya CCM-Kirumba – Mwanza Aprili 1 na kuelekea kule Simiyu Aprili 2 ndani ya Uwanja wa Halmashauri.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.